Romans 3:10-12

10 aKama ilivyoandikwa: “Hakuna mwenye haki, hakuna hata mmoja.

11 Hakuna hata mmoja mwenye ufahamu,
hakuna hata mmoja amtafutaye Mungu.

12 bWote wamepotoka,
wote wameoza pamoja;
hakuna atendaye mema,
naam, hakuna hata mmoja.”
Copyright information for SwhKC